Sunday, May 28, 2017

Rais Magufuli amemtembelea mzee aliyechora Nembo ya Taifa

Leo May 28, 2017 Rais Magufuli amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa wodi ya Mwaisela akiwemo Mzee Ngosha aliyeshiriki kuchora Nembo ya Taifa na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa kazi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.

Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth wamewatembelea wagonjwa leo asubuhi wakitokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ambako wamehudhuria ibada ya Jumapili.
Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali na Rais Magufuli na mkewe ni mtoto Shukuru Musa Kisonga ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na Maziwa.
Pamoja na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na changamoto zinazowakabili madaktari na wauguzi.
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment