Thursday, May 18, 2017

KINANA AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI WA KUSINI MWA AFRIKA (FRONT LINE STATE PARTIES).

katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdrahamani Kinana yuko nchini Angola akiongoza ujumbe wa CCM katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya ukombozi wa kusini mwa Afrika( Front Line State parties).

Pia Ndugu Katibu Mkuu ameongoza Majadiliano na vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .

Ujumbe wa CCM umejumuisha katibu wa Itikadi,Siasa na Uenezi( Ndg.Humphrey Polepole) Katibu wa Siasa na Uhusiano wa kimataifa(Ndg.Ngemela Lubinga) na watendaji wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Vyama Rafiki Vimepongeza CCM MPYA NA MWENENDO WAKE.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vyama Rafiki vilivyoshiriki Mkutano huo kikiwemo Chama Cha Kikomunisti Cha watu wa China .


source:issamichuzi
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment