Monday, May 29, 2017

IGP Mangu atemwa, Sirro apewa nafasi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP). Kabla ya Uteuzi huo, IGP Simon Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilieleza jana kuwa IGP Sirro ataapishwa saa 3:30 asubuhi Ikulu Dar es Salaam leo.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, IGP Sirro alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na baadaye Julai 2011, alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam, kuwa Kamanda wa Kikosi cha Operesheni Maalumu iliyokuwa imeachwa wazi na Kamanda Venance Tossi aliyestaafu. Desemba 2015, IGP Sirro aliteuliwa kuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam akichukua nafasi ya Suleiman Kova aliyestaafu.

source:habarileo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu

0 comments:

Post a Comment