Friday, March 10, 2017

Rais Dkt. Shein asema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wa jana.

Dkt. Shein ametoa msimamo huo  katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi akiwakilisha Rais John Magufuli ambapo amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yeyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein katika mazungumzo yake na vyombo vya habari    alilezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema mkutano huo utaleta tija na faida kubwa kwa wazanzibari na watanzania  katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii,uvuvi,ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya  na  ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi  huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.



0 comments:

Post a Comment