Thursday, March 16, 2017

Issa Hayatou avuliwa Urais CAF, Ahmad Ahmad wa Madagascar ashinda kwa kishindo

Hatimaye Ahmad Ahmad kutoka nchini Madagascar amefanikiwa kumbwaga aliyekuwa Rais wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Issa Hayatou katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo nchini Ethiopia.
Katika uchaguzi huo Ahmad ameshinda kwa jumla ya kura 34 dhidi ya kura 20 alizopata Issa Hayatou. Hayatou alikalia kiti hicho cha urais kuanzia Machi 10 mwaka 1988 ikiwa ni takribani miaka 29.
Wakati huo huo ombi la Zanzibar kuwa mwanachama mpya wa shirikisho hilo limepitishwa bila kupingwa na kufanya jumla ya wanachama kwenye shirikisho hilo kufikia 55 mpaka sasa.


0 comments:

Post a Comment