Baada ya Nape Nnauye kuzuiliwa kufanya mkutano na waandishi wa Habari kisha kutolewa Bastola mbele ya waandishi wa habari na kurudishwa kwenye gari.
Tukio hilo liliendelea kuwa mjadala kwenye mitandao ya mbalimbali ya kijamiii ambapo leo March 24 20017 Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameyaandika haya baada ya tukio hilo.
‘Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini’
“Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake- Mwigulu

Source:millardayo
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.
0 comments:
Post a Comment