Tuesday, February 7, 2017

Halima Mdee amtetea Wema

Wabunge wa upinzani Jumatatu hii wameikosoa vikali njia aliyoitumia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwajumuisha mastaa wakiwemo Wema Sepetu kwenye orodha yake.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amedai kuwa kinachofanyika ni ‘usanii’ kwakuwa anaamini Makonda anawajua vyema mapapa wa biashara hiyo wanaotakia kutajwa na sio kuwakamata akina Wema.
Mdee alimuingiza pia Makonda kwenye picha na kuikosoa safari yake ya siku 20 nchini Marekani huku akihoji nani aliifadhili. “Hakuna anayejua aliyemfadhili kwa siku 20, hana ubavu wa kuishi Marekani siku 20. Inawezekana hawa wauza unga ndio wanampeleka huko, anakuja anawakamata akina Wema, Wema kweli?”
“Alizunguka na nyie kwenye kampeni mlikuwa hamjui? Alikuwa na makamu wa Rais, miezi mitatu sijui mama na mtoto, mkapata kura za mateenagers kupitia huyo mtoto, kwahiyo siku zote kumbe ananusa kitu kama wa rais hajui!”
Wabunge wengine wa upinzani nao wamekosoa njia iliyotumika.



0 comments:

Post a Comment