Baada ya uvumi kusambaa kila kona na kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Beyonce kutohudhuria Coachella, Sasa taarifa imesibitishwa kwamba Beyonce amesitisha kuhudhuria kwenye Coachella.
Taarifa hiyo ya Beyonce kuhusu kutohudhuria kwenye Coachella imetolewa kupitia Parkwood Entertainment pamoja na producer Goldenvoice, ujumbe ulikuwa unasema kwamba “Following the advice of her doctors to keep a less rigorous schedule in the coming months, Beyoncé has made the decision to forgo performing at the 2017 Coachella Valley Music & Arts Festival.”
Licha ya kutohudhuria katika tamasha hilo, waandaji wa wamesema kwamba wamempa Beyonce nafasi nyingine mwakani, kama utakumbuka mwanzo wa mwezi huu Beyonce aliamua kuwapa suprise mashabiki wake kwa kusema kwamba yeye na mumewake Jay z wanatarajia kupata watoto mapacha, “We would like to share our love and happiness. We have been blessed two times over, We are incredibly grateful that our family will be growing by two, and we thank you for your well wishes.”
Mpaka sasa mashabiki wamekuwa na wasi juu ya atakayechukua nafasi ya Beyonce katika tamasha hilo ambalo Beyonce anasubiriwa kwa hamu zote baada ya kutangaza kuwa atakuja na suprise ya wasanii wengine ndani ya tamasha hilo la Coachella.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment