Klabu ya Tottenham imefutilia mbali ndoto ya Chelsea kutaka kuweka historia katika ligi kuu ya England kwa kushinda michezo 14 baada ya vinara hao kufungwa 2-0 White Hart Lane.
Spurs wamesogea mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya mchezaji Dele Alli kufunga magoli yote mawili kwa njia ya kichwa hii ikiwa ni mwishoni mwa kipindi cha kwanza na dakika ya 54.
Alli alifunga vyema kwa kupokea pasi safi kutoka kwa Christian Eriksen kwa magoli yote mawili.
Eden Hazard alikosa nafasi mbili za kuiokoa Chelsea lakini Spurs waliweza kufanikiwa kaupata point tatu muhimu na kuwaondoa majirani zao Arsenal katika nafasi ya nne.
Source:bongo5
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment