Wednesday, January 4, 2017

NAY, NINAWEZA KUWASAIDIA MASHABIKI KUWATOFAUTISHA DIAMOND NA ALIKIBA


Baada ya kuachia ngoma yake ya “Sijiwezi” ambayo inafanya vizuri kwa sasa kwenye Industry ya muziki, Nay ameamua kufunguka na kuiweka tofauti ya Diamond pamoja na Alikiba kwa kutumia jambo hili ambalo najua mashabiki wa muziki wanaweza kuungana na Nay.
Akiongea na Planet Bongo Nay amefunguka na kusema kwamba katika wasanii wakubwa watatu Tanzania wazuri wa kwanza atakuwa ni Alikiba na likija swala la Wasanii watatu wakubwa Wafanya biashara Tanzania Diamond Platnumz kwake ni wa kwanza.
“Watu wanajenga picha kuwa mimi na Alikiba siwezi kufanya naye kazi sababu tu ya uswahiba wangu na Diamond ni kweli Alikiba si mshikaji wangu lakini leo hii ukiuliza nikutajie wanamuziki watatu wazuri Tanzania wa kwanza nitamtaja Alikiba, lakini pia ukisema nitaje wasanii watatu wakubwa wafanyabiashara basi nitamtaja Diamond Platnumz” alisema Nay wa Mitego.

Source:perfect255
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video


0 comments:

Post a Comment