Baada ya kuwa na malumbano kati ya Mr T Touch na Nay wa Mitego kuhusu maswala ya studio na ngoma ambazo wamefanya, T Touch ameamua kufunguka na kusema kwamba Nay wa mitego ni Pretender.
Kupitia kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm, Mr T Touch ameamua kufunguka maswala yake na Nay wa mitego kwa kusema kwamba vitu ambavyo vimefanya yeye na Nay watengane ni vitu ambavyo Nay anavifahamu kwa undani kabisa na wala sio hivyo ambavyo Nay amekuwa akiongea kuhusu Mr Touch kwasababu Nay anaogopa kujizalilisha katika jamii.
“Nimekesha sana na Nay toka mwaka 2012, mwaka wa tano sasa tumekuja kutengana mwaka jana, kitu ambacho kimefanya nitengane naye sio vitu ambavyo yeye anavizungumzia, ni vitu ambavyo yeye mwenyewe anajua ukweli lakini hataki kuongea ukweli kwasababu hataki kujizalilisha kwenye jamii, ila kitu kikubwa ambacho anatakiwa kujua ni kusamini mchango wa Producer,…Mi sikatai kwamba nimeanza kufanya kazi na Nay ndio nikaanza kufahamika ilo jambo siwezi kulikataa, kwasababu ni mchango wake, “ Alisema Mr T Touch.
Ishu hiyo imekuja baada ya Nay wa Mitego kusema kwamba Studio ni mali yake na ataendelea kutumia beats zote zilizopo na ukiendelea kumfuata fuata sana atamwonyesha, ndipo Team ya XXL ikaona kwani shiling ngapi ikiwa na Mr T Touch kujua tatizo liko wapi.
T Touch aliendelea kufunguka kwa kusema kwamba “Producer hajawahi kulipwa na msanii, producer huwa alipwi hiyo ni hati miliki ya mtu otherwise nikupe mkataba wa kukulisisha hicho kitu, biti ni kama urithi, biti producer ni kama anakodisha….kama hiyo sheria ya muziki haijui anapaswa kuongea hivyo, kama anaijua inamaana yeye ni msanii mkubwa lakini haijui sheria ya muziki jinsi ilivyo….studio ni yake ila biti sio yake ndio maana ana studio nyumbani kwake ila haitengenezi biti…studio ambayo nafanya nayo kazi sasa sio mali ya Nay wa mitego” Alisema Mr T Touch.
Wakati Mr T Touch akiwa anaendelea kufunguka kuhusu Nay wa mitego, Nay hakuona shida kupiga simu ya moja kwa moja ndani ya Kipindi cha XXL kwa kufunguka naye makubwa ambayo alitaka waTanzania wote wafahamu kuhusu Ishu hii ya maswala ya studio na Biti.
“Brother mi na Mr T hatukuwa na argument yeyote ile, hatukuwa na argument yeyote ile, Brother wanasema mfadhili mbuzi utamla mchuzi ila sio binadamu, hivi vinavyotokea sahivi mwenyezi mungu atasimama kujua nani alitenda haki,..Mimi hatukuwa na makubaliano yeyote, studio ya Free nation ni ya kwangu na inafahamika hivyo, nilimwambia fanya kazi, miaka miwili mitatu sijawahi kumdai shilingi kumi, mimi nikienda narekodi nyimbo zangu naondoka, sasa ubinadamu huo msanii gani anaweza kuufanya, ningekuwa namlipa laki tatu kila nyimbo kama wasanii wengine wanavyofanya, ubinadamu huo nani anaweza kuufanya…leo unakuja kuletewa lawama kwamba mimi nilikuwa simlipi..hatukukubaliana hata siku moja tulipane,….nimefungua studio mimi ndio nilikuwa nalipa kodi nafanya kila kitu hapo..yeye kazi yake ni kurekodi na kinachoingia ni cha kwakwe, leo unakuja kumlaumu mtu kwamba alikuwa hakulipi,..mimi ilikuwa inafika time siingii studio mwezi mzima, sijawahi kumuuliza nyimbo zote zinazo hits umeingiza shilingi ngapi…sijawahi kujua,..hii ni game ya muziki tutaona mwisho wa hili” Aliongea Nay wa Mitego kwenye Simu.
Source:perfect255
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
0 comments:
Post a Comment