Monday, December 5, 2016

MOURINHO AJITETEA KWA KUMCHEZESHA FELLAINI DHIDI YA EVERTON

Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa
kumuingiza uwanjani kiungo wa kati Marouane Fellaini kama nguvu mpya wakati wa mechi ambayo Manchester United walitoka sare na Everton Jumapili.
Fellaini alisababisha penalti muda mfupi baada yake kuingia dakika ya 85, na kuwawezesha Everton kusawazisha na mambo yakawa 1-1.
Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake, Mourinho
alisema alimwingiza kwa sababu ya kimo chake na uchezaji wa Everton.
“Nilifikiri kwamba mnafaa kuwa mnajua mengi zaidi kuhusu soka kuliko mlivyo,” Mourinho alsiema akiongea na wanahabari.
“Everton si timu ya kutoa pasi kama walivyokuwa zamani. Everton ya sasa ni klabu inayocheza moja kwa moja: kipa moja kwa moja, Ashley Williams moja kwa moja, Ramiro Funes Mori moja kwa moja. Kila kitu moja kwa moja.

“Unapokuwa na mchezaji wa kimo cha mita mbili kwenye benchi unamchezesha kwenye safu ya ulinzi kuisaidia timu kushinda mipira.” alimalizia

Source:perfect255

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video





0 comments:

Post a Comment