Hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameianza ziara yake ya siku kumi kwa Wilaya Tano za Mkoa huo, huku lengo kubwa ikiwa kutatua kero za wananchi waishio jijini humo na kupatikana kwa Dar Mpya yenye kumpendeza na kumnufaisha kila mtanzania.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Wilaya ya Kigamboni ambapo ndiyo wilaya aliyoanza nayo, Mkuu wa Mkoa huyo RC Makonda amesisitiza uwajibikaji wa kila mtendaji wa seriklali na kufafanua kuwa kila mtumishi akiwajibika kwa nafasi yake yatafikiwa malengo ya kupatikana Dar Mpya yenye tija kwa Taifa kwa ujumla, pia ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuongeza uwajibikaji kwa watumishi na kuyatekeleza yale yaliyo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika hatua nyingine RC Makonda amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigamboni Steven Katemba kuhakikisha watendaji wanasikiliza kero za wananchi na kutoa ripoti kila wiki ya kero zilizosikilizwa, kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashimu Mgandilwa amemuomba RC Makonda kuwaombea eneo la Ofisi za Wilaya kwani kwasasa wanaofisi nane katika maeneo tofauti, hivyo wamemuomba kuwaombea nyumba iliyoachwa na hayati Aboud Jumbe ambayo ilikuwa inatumiwa na watu wa usalama wa Taifa, huku akizitaja changamoto nyingine kuwa ni uvuvi haramu, gari la zima moto,,upungufu vyumba vya madarasa, miundombinu ya maji safi na maji taka.
Akijibu changamoto hizo RC Makonda amehaidi kuwasiliana na viongozi wa usalama wa Taifa ili kuwaombea jengo lililoacha na hayati Aboud Jumbe ili walitumie kama ofisi, pia amepiga marufuku uchimbaji wa kokoto kwa eneo la Mji Mwema kwani unachochea uharibifu wa Mazingira,hatarishi kwa usalama wa wakazi waishio maeneo , pia maeneo hayo yanaweza kutumika kwa vitendo vya uhalifu.
Source:mtembezi
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter naInstagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
0 comments:
Post a Comment