Tuesday, November 15, 2016

TUKIO LA MWEZI KUISHANGAZA DUNIA LEO

Leo ni katikati ya mwezi Novemba, zimesalia siku 46 kuumaliza mwaka 2016 ambao umesheheni mambo kadha wa kadha; sasa lengo kuu sio kuuzungumzia mwaka huu nini kimetokea kubwa ni kuhusu tukio la kihistoria linalotazamiwa kutokea usiku wa leo ambapo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Shirika la Masuala ya Anga ya Marekani (NASA) ni kuwa tukio la mwezi kuwa na muonekano wa karibu zaidi kutoka angani na kuwa mkubwa maarufu kama ‘Super Moon’ si la kihistoria kwa mwaka huu pekee bali pia ni historia kuu ya karne ya 21.

Aidha wanasayansi wanadai kuwa muonekano huo wa karibu wa mwezi uliwahi kutokea miaka 70 iliyopita na vilevile muonekano huo wa karibu hautaonekana tena hadi  Novemba 24 mwaka 2034.

Baada ya miaka 68 kwa mara ya kwanza utaonekana kwa ukubwa wa asilimia 14 zaidi huku mwanga ukiongezeka kwa asilimia 30 zaidi. Usiku wa leo kunatarajiwa kuonekana mwezi mkubwa zaidi unaotambulika na wanasayansi kama ‘Super Moon’.

Unaweza kujionea picha za namna mwezi unavyotarajiwa kuonekana usiku wa leo hapa chini.







Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment