Siku chache baada ya Rais John Magufuli kusema kuna utoroshaji mkubwa wa madini kupitia viwanja vya ndege vilivyopo migodini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umekamata madini yenye thamani ya Sh3,353,421,381.4 yakitoroshwa katika viwanja vikubwa vya ndege na katika matukio 25 tofauti.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMAA, Mhandisi Dominic Rwekaza ameeleza hayo kwenye ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na wakala huo mwaka 2015.
“Katika kufuatilia usafirishaji wa madini nje ya nchi katika viwanja vikubwa tulikamata madini yanayotoroshwa yenye thamani ya Dola za Marekani 1,512,186.61 na mengine ya Sh34,670,794 katika matukio 25 tofauti.”
Source:mtembezi
0 comments:
Post a Comment