Kwa kawaida mara Uchaguzi Mkuu unapomalizika kwa nchi yoyote mengi huzungumzwa na rapsha rapsha za hapa na pale vuta ni kuvute ni mambo ya kawaida kama ulimwengu ulivyoshuhudia kile kilichokuwa kikiendelea hivi karibuni nchini Marekani mara baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa na Donald Trump kuibuka na ushindi hali iliyowafanya wananchi wa taifa hilo kuandamana huku wengine wakikana kumtambua kama rais wao.
Yaliyopita si ndwele kwa kuwa Trump ameamua kutupa karata yake ya kwanza kwa kufanya uteuzi kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe; Reince Priebus ndiye aliyebahatika kuwa chaguo la kwanza kwa kupewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Chama cha Republican akitumika kama Mkuu wa Wafanyakazi.
Mwingine ni Stephen Bannon aliyekuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Breitbart News, ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia, yeye ameteuliwa kushika nafasi ya Mkuu wa Mipango na Mshauri Mwandamizi.
Hata hivyo taarifa zinasema uteuzi alioufanya Trump kwa Priebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini kwa kuwa kiongozi huyo anauhusiano wa karibu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan. hali inayoashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na Baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Source:mtembezi
0 comments:
Post a Comment