Monday, November 14, 2016

DHAMANA YA LEMA KUJULIKANA LEO

Mbunge wa jimbo la Arusha, Godbless Lema(40)  na Mkewe Neema Lema(33)  wanatarajia tena kupanda kizimbani leo kwa madai ya kesi ya uchochezi  dhidi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ijumaa wiki iliyopita Lema alipelekwa gereza la Kisongo Arusha, kutokana na kunyimwa dhamana, katika kesi nyingine ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli hatua ambayo imepingwa na chama chake na mawakili wake.

Hata hivyo Chadema  kinatarajia kuwasilisha maombi mahakama kuu, kuomba Lema apewe dhamana.

Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alisema jana kuwa hawakuridhishwa na pingamizi la dhamana lililowekwa na mawakili wa serikali wiki iliyopita kwani tayari Lema alikuwa amepewa dhamana na hakimu.

“Tayari tumefanya mazungumzo kuongeza nguvu za mawakili wa chama ambao wataungana na mawakili wa Arusha kudai dhamana leo”alisema.

Naye Wakili Shaki Mfinanga alisema leo watawasilisha maombi ya dhamana ya Lema wakiwa na mawakili wa Chadema.

“Taratibu za kisheria zinaendelea tunatarajia jumatatu kuwasilisha pingamizi la Lema kunyimwa dhamana.”alisema


Source:mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video






0 comments:

Post a Comment