Sunday, October 30, 2016

YANGA YAILIPA SIMBA YAIPUMILIA KISOGONI

Ligi kuu ya Tanzania bara inazidi kuyoyoma na sasa ubabe wa Simba na Yanga unazidi kudhiihirisha katika mechi zao za ligi hii tamu kabisa. Simba walipata ushindi ugenini lakini Mbao Fc waliwasumbua mechi ya kwanza na walisubiri hadi dakika ya 84 kupata ushindi.

Yanga wamesubiri kipindi cha kwanza tu baada ya kipindi cha pili Yanga walikuja kasi na kuonesha kutaka ushundi  kitaalamu waliwaweza Mbao licha ya kucheza vizuri tena kwa kandanda safi huku Asante Kwasu akiwa kivutio uwanjani.

Yanga walipata bao la kwanza kupitia kwa Vicent Basou kwa kichwa kabla ya Mbuyu Twite akirusha mpira  na kipa kuudumbukiza nyavuni, lakini Amisi Tambwe akasema sikubali ngoja nimfuate Kichuya akaweka goli la tatu .

KIVUTIO

Mwinyi Haji ndiyo nyota wa mchdzo na aliitwa Marcelo kwa aina ya uchezaji wake pamoja na kandanda safi huku Niyonzima kama kawaida yake kupiga mipira huku akiangalia pembeni na beki wa Mbao Kwasu akicheza kwa ustadi mkubwa dakika zimekata Yanga 3 Mabao 0.




Source: mtembezi

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video




0 comments:

Post a Comment