Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za wizi wa miundombinu ya umeme yenye thamani ya milioni 61 ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamshna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, DCP Lucas Mkondya amesema jana kikosi kazi cha kuzuia uharibifu wa miundombinu cha Tanesco kwa kushirikiana na polisi baada ya kupata taarifa za wizi wa miundombinu kutoka kwa raia wema.
Kilifanya upekuzi katika nyumba ya Wilfred Baruti mkazi wa Makumbusho na kukuta vifaa vya wizi vya kuunganishia umeme .
Pia kilifanya upekuzi katika nyumba ya Beatrice Emanuel mkazi wa Salasala na kukamata vifaa vya umeme.
DCP Mkondya amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na upelelezi utakapo kamilika watapelekwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Pia DCP Mkondya amesema Kikosi Maalumu cha Kupambana na Uhalifu cha kanda ya Dar es Salaam kimekamata watuhumiwa wawili wakiwa na funguo bandia 75 kwa kosa la uvunjaji nyumba za biashara, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ally Makwega mkazi wa Tandika na Fabian Greyson mkazi wa Yombo.
0 comments:
Post a Comment