Kufuatia changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano la Vijana lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.
Pia amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Read More
0 comments:
Post a Comment