Bingwa wa ngumi uzani mzito wa duniani, Mwingereza Tyson Fury amepewa siku 10 na WBO kueleza ni kwa nini hafai kupokonywa mkanda wake wa ubingwa.
Baada ya kujiondoa kutoka kwa pigano lake la marudiano na Wladimir Klitschko wa Ukraine mapema mwezi huu kwa sababu ya matatizo ya kiakili.
Bondia huyo ambaye ana miaka 28 pia anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa zisizoruhusiwa.
Bondia huyo ambaye ana miaka 28 pia anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa zisizoruhusiwa.
Kwenye mahojiano na runinga moja wiki iliyopita, alikiri kutumia kokeini kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mwenyekiti wa WBO Luis Batista-Salas amesema Fury huenda akapoteza mkanda huo kwa “kutoshiriki mapigano, kuvunja mkataba na kwa kutumia dawa zilizoharamishwa.”
Mwenyekiti wa WBO Luis Batista-Salas amesema Fury huenda akapoteza mkanda huo kwa “kutoshiriki mapigano, kuvunja mkataba na kwa kutumia dawa zilizoharamishwa.”
Hata hivyo amesema WBO wanajali sana hali yake ya kiafya na wanamtakia afueni ya haraka.
Fury ndiye pia bingwa wa WBA.
Fury ndiye pia bingwa wa WBA.
Fury hajapanda ulingoni tangu amshinde Klitschko Novemba mwaka jana.
Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video
0 comments:
Post a Comment