Wednesday, October 5, 2016

Maagizo ya Rais wa Nigeria kuhusu kupigwa mnada ndege za Rais


October 5, 2016 Nakusogezea hii kutoka Nigeria mtu wangu. Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa agizo kwa mamlaka ya usafirishaji nchini Nigeria kuzipiga mnada ndege mbili zinazotumika na Rais wa nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za Umma na ubadhirifu serikalini.


Kwa mujibu wa shirika la habari AFP limezungumza na msemaji wa Rais wa Nigeria, Garba Shehu, ambaye amesema ndege hizo mbili kati ya 10 zinazotumiwa na rais wa nchi hiyo zitauzwa kama sehemu ya kubana matumizi yasiyokuwa na ulazima.
Serikali ya Nigeria imeweka tangazo magazetini kwamba inauza ndege hizo mbili, moja ikiwa ni aina ya Falcon 7X na nyingine ni Hawker 4000.
Taarifa ya msemaji wa Rais inasema Buhari mwenyewe ndiye aliyeidhinisha kuuzwa kwa ndege hizo huku akitoa agizo kuwa baadhi ya ndege nyingine za rais zikabidhiwe kwa jeshi la anga la nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment