Nick wa Pili alikuwa mmoja wa wale watoto waliojua kusoma na kuandika (walau wa uchache) kwa kufundishwa tu nyumbani kabla ya kuanza shule rasmi.
Na ni kaka yake, Joh Makini ndiye alikuwa mwalimu wake wa kwanza.
“Joh Makini kwanza ndiye aliyenifundisha kusoma na kuandika kabla ya kuanza darasa la kwanza,” Nick alimwambia Prince Ramalove wa Kings FM.
Pamoja na kukiri kuwa kaka yake ni kichwa, haoni kama angependa kuja kuwa mwalimu.
“Sijui kama hicho kilikuwa ndani yake, lakini naona ni mtu mwenye akili sana, sijui nitamweka wapi lakini kama asingekuwa msanii angekuwa anafanya kitu kingine tu,” alieleza.
Nick wa Pili ni msomi wa shahada ya uzamili kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment