Sunday, September 25, 2016

Baada ya talaka na Brad Pitt, Angelina Jolie kuhamia kwenye mjengo huu (Picha)


Baada ya Angelina Jolie kumtandika ‘jab’ ya talaka mumewe Brad Pitt, anahamia kwenye mjengo uliopo pembezoni kabisa mwa Malibu – akibeba na wanae wote, sita.
Kwenye nyumba hiyo ya kifahari, Angie atakuwa akilipa $95,000 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 209 kwa mwezi).
Inadaiwa kuwa muigizaji huyo alipanga kwenye nyumba hiyo yenye thamani ya $12m, wiki tatu kabla ya kudai talaka toka kwa Pitt.

Ina ukubwa futi za mraba, 4,409, ikiwa na vyumba vitano na mabafu matano na itatumiwa na yeye na watoto wao, Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, mapacha Vivienne na Knox, 8.

Jolie na Pitt walianzisha uhusiano mwaka 2004 wakati wakishoot filamu ya Mr. & Mrs. Smith, wakati huo Brad alikuwa amemuoa Jennifer Aniston.

Hizi ni picha zaidi za nyumba hiyo:










0 comments:

Post a Comment