Saturday, August 12, 2017

Wallace Karia Rais mpya TFF

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.
Rais mpya wa TFF ni Wallace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya na wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo.
Karia amewashinda Iman Madega, Shija Richard, Ally Mayay, Emanuel Kimbe na Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.
Karia ataongoza shirikisho la soka Tanzania kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba ya TFF.
Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment