Saturday, July 1, 2017

Watanzania tumechezewa mno- Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema huu ni muda wa kuibadilisha Tanzania huku akisema Watanzania wamechoka kuchezewa katika maendeleo wamechezewa siku nyingi mno.
Akizungumza leo wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba, Rais amesema maonyesho hayo yatumike kama chachu ya maendeleo kwa Watanzania.
“Nadhani huu ni wakati wa kuibadilisha Tanzania, Tumechoka tumechezewa siku nyingi mno, hatujaamka na mimi nawaambia Watanzania tumechezewa mno lakini tulichezewa kwasababu tuliamua sisi kuchezewa ni lazima tubadilike Consious ni kuitengeza Tanzania mpya tuanze nayo sasa,” alisema Rais Magufuli.
Na Emmy Mwaipopo

Tuandikie Maoni Yako Hapa Chini. Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video za kufurahisha na kuvunja mbavu.

0 comments:

Post a Comment