Thursday, November 17, 2016

Nchemba awataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahamiaji wasio rasmi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba leo ameendelea na ziara yake ya kukagua taasisi zilizochini ya wizara yake ambapo ametembelea makao makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Waziri Nchemba katika ziara yake hiyo, ameendelea kuwasisitiza wananchi kuwafichua wageni wanaoishi nchini kinyume cha sheria baada ya kubaini kuwa wahamiaji haramu bado tatizo.
Katika ziara yake ya jana kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji alibaini kuwa kuna ongezeko la wahamiaji haramu pamoja na raia wa kigeni kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kupata urai na vitambulisho vya taifa.
“Natoa wito kwa wananchi kwamba wanapobaini kuna raia wa kigeni watoe taarifa kwa mamlaka husika, kumejengeka tabia baadhi ya watu hufichua raia hao kwa masilahi yao binafsi na kwamba pasipo masilahi yao kuguswa hawasemi wanawaacha wanapata haki za msingi kama raia,” amesema.
Hata hivyo, amewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la uandikishaji na utoaji wa namba za utambisho linalotarajiwa kuamza mwezi Disemba mwaka huu. Pia ameitaka NIDA kuendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi.
“Mnajukumu katika kuhamasisha wananchi kwa ajili ya zoezi la utambuzi na uandikishwaji wa kupata vitambulisho,” amesema.
Amesema vitambulisho vipya vitakavyotolewa vitamsaidia mwananchi kutambulika popote pia vitaondoa udanganyifu.
“Vitambulisho hivyo vitakua vya kielektroniki, na kila mwananchi atatia saini ya alama za vidole hivyo si rahisi mtu kufanya udanganyifu,” amesema.

Source:dewjiblog

Jiunge na hatukwamii.blogspot.com/ sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video



0 comments:

Post a Comment