Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amezitaka benki na taasisi za kifedha nchini kujenga viwanda na kuvikopesha kwa vikundi vya wajasiliamali ili wajikwamue kiuchumi pamoja na kuongeza idadi ya viwanda.
Mwijage ameyasema hayo wakati akifungua maonyesho ya 10 ya MOWE katika viwanja vya MnaziMmoja jijini Dar es Salaam.
“Benki ya Convenant wamenifurahisha, wamejenga kiwanda cha kuchakata maziwa Songea na kukopesha wakulima kiwanda hicho kitazalisha lita 10,000 kila siku. Natoa wito kwa benki zote nchini waige mfano wa Covenant Bank,” amesema.
Pia amezitaka benki kukopesha wajasiliamali hasa akina mama kwa kuwa wengi wao ni wainifu ni si rahisi kukimbia na madeni
“Wanawake sio kweli kama hawakopesheki, mabenki mtafute mfumo wa kukopesha akina mama sababu ni waaminifu. Benki ya
BOA wameniambia watu wakijiunga katika vikundi watatoa mikopo. Wenye vikundi njooni ofisi kwangu nitawapeleka benki ya BOA ,” amesema.
Amezitaka Halmashauri zote nchini kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda na wajasiliamali.
Mwijage ameahidi kuwa serikali itaboresha miundombinu maeneo ya vijijini ili kuvutia wawekezaji.
“Serikali itapeleka miundombinu wezeshi na saidizi ili kuwawezesha wananchi pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo mawasiliano hivyo ndivyo tutajenga uchumi wa viwanda.
Niwahimize watanzania tukubaliane kwamba tuende pamoja, nchi zote zilianza hivi, wenzetu wametuacha nyuma na sisi tukijikaza tutafika,” amesema.
Source: dewjiblog

0 comments:
Post a Comment