Monday, September 26, 2016

DOKII ASEMA KUIGIZA NAFASI YA UMALAYA, ULEVI SI DHAMBI

Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ mwigizaji wa filamu wa kike mkongwe amefunguka kwa kusema kuwa msanii anapoigiza sehemu inayohusu ulevi au ukahaba haina maana ndio tabia yake halisi.



Ila huwa ni uhusika tu ambao ni njia mojawapo ya kuionyesha athari ya matukio hayo wala si tabia ya mhusika.
Akipiga story na filamu central Dokii alisema “Unapopewa nafasi ya kuigiza kama Kahaba au mlevi ukiangalia imani yako inakuwa ngumu lakini ukiangalia majukumu yanayokuzunguka, ni lazima uigize kwani una watoto wanahitaji ada, kwa hiyo kuigiza nafasi hizo si dhambi”
Dokii anasema kuwa kuna wakati kuna watu
wanaweza kuhoji kuwa Yule ameokoka lakini
mbona anaigiza katika nafasi zile ambazo ni mbaya.
Lakini wanasahau kuwa inawezekana ikawa ni sehemu ya uhubiri na hatupaswi kuwachukia walioanguka katika dhambi bali kuwaombea na kuwafundisha warudi katika njia iliyo sahihi.

0 comments:

Post a Comment